1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aondosha wanajeshi majimboni

Sekione Kitojo
30 Julai 2020

Utawala wa Trump umekubali kuwaondoa wanajeshi iliowatuma jimboni Portland, ambao kuwapo kwao kumewakasirisha waandamanaji kwa lengo la kupunguza wiki kadhaa za  makabiliano katika mji huo.

US-Präsident Donald Trump
Picha: picture-alliance/AP Photo/E. Vucci

Gavana wa mji  wa Oregon, Kate Brown, alisema  majeshi ambayo  uwekwaji  wake ulionekana na wengi kama sehemu ya kaulimbiu mpya ya Rais Donald Trump ya "amani na sheria", ambayo inahusishwa na kampeni za kutaka kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi wa Novemba, wataanza kuondolewa kwa awamu kuanzia leo (Julai 30). 

Hata hivyo, Kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani, Chad Wolf, aliashiria kuwa wanajeshi hao wataondolewa iwapo tu kutakuwa na uhakikisho kuwa polisi wa mji huo watahakikisha jengo la Mahakama ya Juu ya Shirikisho litakuwa salama. 

Mapema mwezi juu, utawala wa Trump ulituma wanajeshi kuingilia kati katika mji huo, baada ya wiki kadhaa za maandamano dhidi ya ubaguzi na ukatili  wa polisi kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika, ambazo zilishuhudia madirisha yakivunjwa na jengo la Mahakama ya Juu ya Shirikisho na majengo mengine kuchafuliwa kwa rangi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW