1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aonya Israel kutoingilia masuala ya Syria

2 Desemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump aliionya Israel dhidi ya kuisababishia machafuko Syria na uongozi wake mpya, siku chache baada ya operesheni iliyosababisha vifo iliyotekelezwa na vikosi vya Israel kusini mwa nchi hiyo.

Syria Beit Jin 2025 | Pikipiki iliyoharibiwa baada ya shambulio la kijeshi la Israel
Mwonekano wa pikipiki iliyoharibika baada ya shambulio lililofanywa na jeshi la Israel katika kijiji cha Beit Jin, kilichoko eneo la Qatana katika vitongoji vya Damascus kusini mwa Syria Novemba 28, 2025Picha: Bakr Al Kasem/Anadolu Agency/IMAGO

Kupitia mtandao wake wa kijamii  Truth Social, Rais Trump ameandika  "Ni muhimu sana Israel kudumisha mazungumzo madhubuti na ya kweli na Syria, na kuhakikisha hakuna kinachofanyika kitakachozuia mabadiliko ya Syria kuwa taifa lenye ustawi." Trump amekuwa akisisitiza juu ya makubaliano ya usalama kati ya Israel na Syria tangu kuangushwa kwa mtawala wa muda mrefu Bashar al-Assad mwaka mmoja uliopita. Hata hivyo, mvutano umeongezeka kutokana na mamia ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria. Katika shambulio la kifo vingi hadi sasa, vikosi vya Israel viliua watu 13 Ijumaa katika operesheni kusini mwa Syria, wakisema walilenga kundi la Kiislamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW