Trump apandishwa kizimbani kujibu kesi ya jinai
15 Aprili 2024Huko Marekani, Rais wa zamani wa taifa hilo Donald Trump Donald Trump amepandishwa kizimbani katika mahakama mjini New York kujibu kesi ya jinai inayomkanbili, Trump anakuwa rais wa kwanza wa zamani katika historia ya Marekani kujibu kesi hiyo, Haya yanajiri wakati wimbi la kampeni za uchaguzi mkuu wa urais nchini humo zikiendelea kupamba moto.
Soma zaidi. Kesi ya kwanza ya jinai dhidi ya Trump yaanza kusikilizwa
Jumatatu ya leo, Trump aliongozwa na msafara wa magari hadi kwenye mahakama ya Manhattan kutoka kwenye jengo lake la Trump Tower muda mfupi kabla ya kuchaguliwa kwa jopo la mahakama la kuisikiliza kesi hiyo.
Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 77 anakabiliwa na kashfa ya kughushi rekodi za biashara katika mpango wake wa kuficha madai ya ngono na mwigizaji wa filamu Stormy Daniels ili kujiweka salama na shutuma wakati wa kampeni zake za uchaguzi wa 2016.
Malipo hayo aliyofanya kwa mwingizaji huyo ili kumnyamazisha ni miongoni mwa kesi nne za jinai zinazomkabili Trump, ikiwa ni pamoja na mashtaka ya madai ya kihistoria dhidi ya mgombea huyo wa urais wa chama cha Republican ya kuharibu uchaguzi wa 2020 na kumzuia mshindi, Joe Biden, kuchukua madaraka.
Trump: Kesi hii ni shambulio kwa Marekani
Iwapo atapatikana na hatia katika kesi ya hiyo ya malipo, Trump atakabiliwa na kifungo cha miaka jela, ingawa wataalamu wa sheria wanaona kuwa jambo hilo halitowezekana.
Donald Trump mwenyewe amesema kesi hiyo ni shambulio dhidi ya Marekani.
"Hili ni shambulio dhidi ya Marekani. Hakuna kitu kama hiki, hakijawahi kutokea. Hakuna kitu kama hicho. Kila msomi wa sheria alisema kesi hii ni ya upuuzi, haikupaswa kuletwa. Haistahili kitu kama hiki. Kuna hakuna kesi. Na wamesema hivyo. Watu ambao hawafumfuatilii au kumpenda Donald Trump walisema kuwa haya ni mateso ya kisiasa Na tena, ni kesi ambayo haikupaswa kuletwa Ni shambulio kwa Marekani, nchi ambayo inaendeshwa na mtu asiye na uwezo ambaye anahusika sana katika kesi hii'' amesema Trump.
Siku ya Jumatatu, timu yake ya kampeni ilitoa video ikimuonyesha Trump akiwaeleza wafuasi wake kuwa wapo watu wanaotaka uhuru wake na kwamba atasimama thabiti ili kukabiliana na kesi hiyo.
Kesi hiyo imeanza kwa uteuzi wa jopo la wasikilizaji, kundi la raia wa kawaida walioitwa na Jaji Juan Merchan ambao baadaye watatakiwa kujaza dodoso ikiwa ni pamoja na ukagauzi wa iwapo ni wamewahi kuwa wanachama wa vikundi vya mrengo mkali wa kulia.
Soma zaidi. Wanasheria wataka Mahakama ya Juu kumshitaki Trump
Trump anashutumiwa kwa kumlipa fedha zilizotumwa na wakili wake Michael Cohen kumlipa Stormy Daniels ili kumnyamazisha kuhusu madai ya ngono yaliyotokea siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Mahakama kuu ya New York ilimshtaki Trump mnamo Machi 2023 juu ya malipo yaliyofanywa kwa Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, huku rais huyo wa zamani akishtakiwa kwa makosa 34 ya kughushi rekodi za biashara.
Trump mwenyewe anakanusha mashtaka hayo na anaweza kuitumia kesi hiyo, iliyopangwa kwa hadi miezi miwili, kama jukwaa maarufu la kukashifu kile anachodai kuwa ni "sheria" na kuingiliwa kwa uchaguzi na wapinzani wake wa kisiasa.
Vyanzo; AFP
Mwandishi : Suleman Mwiru.