1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Trump: Iran, Israel zinahitaji 'kupigana' kabla ya kupatana

16 Juni 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amezitaka Iran na Israel, ambazo zinashambuliana "kufikia makubaliano" ya kusitisha mapigano lakini amependekeza kuwa huenda nchi hizo mbili zinahitaji "kupigana" kwanza kabla ya kuafikiana.

USA Washington 2025 | maadhimisho ya miaka 250 ya jeshi la Marekani
Rais Donald Trump katika maadhimisho ya miaka 250 ya jeshi la MarekaniPicha: Carlos Barria/REUTERS

Rais wa Marekani Donald Trump amezitaka Iran na Israel, ambazo zinashambuliana "kufikia makubaliano" ya kusitisha mapigano, lakini amependekeza kuwa huenda nchi hizo mbili zinahitaji "kupigana" kwanza kabla ya kuafikiana.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuelekea Canada katika mkutano wa nchi 7 tajiri kiviwanda za G7, Trump alisema kwamba anafikiri umefika muda kwa nchi hizo mbili kufikia makubaliano, lakini wakati mwingine zinapaswa kupigana kwanza na kuongeza kuwa wataona kitakachofuata.

Trump alikataa kujibu swali iwapo aliitaka Israel kusitisha mashambulizi ya anga dhidi ya Iran. Hapo awali, afisa mmoja mwandamizi wa Marekani aliliambia shirika la habari la AFP kwamba Trump alipinga mpango wa Israel wa kumuua kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

Mashambulizikati ya nchi hizo mbili yamezusha hofu ya mzozo mkubwa ambao unaweza kulikumba eneo zima la Mashariki ya Kati.