1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump apigiwa kura kwa matumizi mabaya ya madaraka

19 Desemba 2019

Baraza la Wawakilishi la Marekani limepiga kura kuridhia kushtakiwa kwa Rais Donald Trump kwa kutumia vibaya madaraka yake na kuingilia uchunguzi wa Bunge.

USA Trump Amtsenthebung
Picha: picture-alliance/AP Photo/House Televiwion

Mchakato wa mwisho wa kura utalihusisha baraza la Seneti ambalo litakuwa na mamlaka ya kuamua kama anaweza kuondolewa madarakani au la

Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: AFP/B. Smialowski

Matokeo ya mchakato huo ulikuwa ulijulikana mapema kutokana na baraza hilo kuwa na wingi wa wabunge wa chama cha Democratic.  Baada ya majadilioano ya masaa 10, wabunge walipigia kura vifungu viwili vya sheria ambavyo  kwa madai ya utumiaji mbaya wa madaraka na uzuiaji wa bunge unaohusiana na shughuli za rais huko nchini Ukraine.

Katika uchaguzi wa mwanzo kati ya michakato miwili, wabunge 230 wa chama cha Democratic waliibuka na ushindi wa wazi ili kufanikisha azma yao dhidi ya Trump,  Ingawa wawili miongoni mwao walipiga kura ya kinyume na wengi. Lakini kwa upande wa chama cha Republican wabunge wote walivipinga vufungu vyote viwili. Baraza la wawakilishi lina nguvu ya kumshitaki rais kwa wingi mdogo wa kura, lakini baraza la Seneti litahitaji wingi wa theluthi mbili kumuondoa rais madarakani, hatua ambayo sio rahisi kufanyika. Rekodi zinaonesha kuwa hatua hiyo ni ya mara ya tatu kwa rais wa Marekani kushitakiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW