1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump aidhinisha "wabadili jinsia" kuondolewa jeshini

28 Januari 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kutia saini msururu wa maagizo, ametia saini agizo kuu la kuwaondoa wanajeshi kutoka kwa kile alichokiita "itikadi ya watu waliobadili jinsia."

USA US-Präsident Donald Trump im Oval Office in Washington
Picha: Carlos Barria/REUTERS

Hatua ambayo wanaharakati wa jamii za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanaona kama ukiukwaji wa haki. 

Katika mfululizo wa maagizo mengine kuhusiana na jeshi, Rais Trump ametia saini amri ya kurekebisha sera jumuishi katika wizara ya ulinzi, ambayo inalenga kuwazuia watu waliobadili jinsia kuhudumu katika jeshi la Marekani.

Katika muhula wake uliopita, Trump alijaribu kuchukua uamuzi kama huo lakini alikabiliwa na vikwazo vya kisheria, na sasa anasema agizo hilo litahakikisha Marekani inakuwa na jeshi imara zaidi duniani.

Soma pia: Wizara ya sheria Marekani yawafuta waendesha mashitaka waliozishughulikia kesi za jinai za Trump

Katika agizo lake, Trump alidai kuwa vikosi vya jeshi "vimekumbwa na itikadi kali za kijinsia ili kuwaridhisha wanaharakati" na kwamba "hali nyingi za kiafya kiakili na hata kimwili haziendani na jukumu la kufanya kazi."

"Nina heshima kubwa kwa jumuiya hiyo. Nafikiri ninaungwa mkono mkubwa au nimepata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa jumuiya hiyo."

"Nilipata kura nyingi kutoka kwao. Lakini mtu aliyebadili jinsia,  imekuwa hali ngumu sana na nadhani ninawafanyia watu wengi neema kwa kujitokeza na kusema tu, limekuwa suala gumu sana kwa jeshi. Na nadhani nimelisaidia pakuwa jeshi kwa upendeleo mkubwa."

Aidha Trumpametoa pia wito wa Marekani kuanzisha mfumo wake wa ulinzi wa makombora unaofanana na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel wa Iron Dome.

Makali na sifa ya vikosi vya jeshi la Marekani

Trump amerejea madarakani na kutanga sera rasmi ya Marekani kutambua jinsia mbili pekee. Alexandria Holder, sajenti wa kiufundi ni mmoja wa waliobadili jinsia katika Jeshi la Wanahewa la Marekani.Picha: Privat

Hakuishia hapo, Trump ametia saini maagizo zaidi ya kuwarejesha kazini wanajeshi waliofukuzwa kazi kwa kukataa chanjo ya UVIKO, na kuzidisha  ukandamizaji mpana wa serikali juu ya mipango anuwai ya wanajeshi.

Katika agizo jengine Trump alidai kwamba mipango mbalimbali katika jeshi "inadhoofisha uongozi, sifa na mshikamano wa vitengo, na hivyo kuondoa makali na utayari wa kutumia nguvu."

Soma pia: Rais Trump aanza awamu mpya kwa kishindo

Pia ilipiga marufuku idara ya ulinzi na vikosi vya jeshi kutangaza kile alichokiita  nadharia za "wasio Wamarekani" zinazopendekeza hati za waanzilishi wa Amerika zina ubaguzi wa rangi au kijinsia au kuendeleza majadiliano juu ya "itikadi ya kijinsia."

Wamarekani waliobadili jinsia wamekuwa wakikabiliwa na mabadiliko makubwa ya sera za utumishi wa kijeshi katika miaka ya hivi karibuni, huku tawala za Kidemokrasia zikitaka kuwaruhusu kuhudumu kwa uwazi huku Trump akisistiza kuwaweka nje.

 

//AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW