1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema amevunjwa moyo na Urusi kuhusu Ukraine

19 Septemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amevunjwa moyo na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kutokubali kusitisha vita nchini Ukraine, akitaja uhusiano wake wa kibinafsi na kiongozi huyo wa Urusi.

USA 2025 | Rais Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: youtube

Katika mahojiano na shirika la utangazaji la Marekani Fox News, Trump pia alikosoa wanachama wa Ulaya wa jumuiya ya kujihami ya  NATO kwa kuendelea kununua mafuta ya Urusi, akisema Urusi itakuwa tayari zaidi kufanya mazungumzo ya makubaliano ya amani ikiwa Ulaya itapunguza uagizaji wake wa nishati kutoka nchi hiyo.

Trump ameongeza  kusema kuwa hatua hiyo ya ununuzi wa nishati ya Urusi sio makubaliano.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW