1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema anapanga kukutana na Putin baada ya kuapishwa

8 Januari 2025

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kwamba anapanga kujadili juhudi za kumaliza vita vya Urusi huko Ukraine na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Marekani I Donald Trump
Rais Mteule wa Marekani Donald TrumpPicha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kwamba anapanga kujadili juhudi za kumaliza vita vya Urusi huko Ukraine na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makazi yake mjini Florida, Trump ameweka wazi kwamba angependelea kufanyika kwa mkutano huo baada ya kuapishwa kwake mnamo Januari 20.

Soma pia: Congress yathibitisha ushindi wa Trump

Trump pia ameongeza kuwa anayo matumaini yake kwamba vita hivyo vya Urusi na Ukraine vitamalizika ndani ya kipindi cha miezi sita. Itakumbukwa wakati wa kampeni zake rais huyo mteule alisema kwamba atavimaliza vita hivyo ndani ya kipindi cha saa 24.

Vita kati ya Urusi na Ukraine vinaelekea mwaka wa tatu sasa na Ukraine inahofia kwamba Trump atakapoingia madarakani Januari 20, msaada inaoupata kwa Marekani unaweza kupungua kwa kasi. Wakati wa hotuba yake ya Mwaka Mpya, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa mwito kwa Washington kutopunguza misaada kwa nchi yake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW