1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema Harris anaiangamiza Marekani

28 Oktoba 2024

Mrepublican Donald Trump amefanya mkutano wa kampeni mjini New York kwa kumshambulia mpinzani wake wa Democratic Kamala Harris. Harris amesema Wamarekani wanapaswa kufanya uamuzi wa busara siku ya uchaguzi.

Marekani I New York City - Donald Trump azungumza Madison Square Garden
Kwenye hotuba yake ya Madison Square Garden, Trump alimshutumu Harris kwa kuiharibu MarekaniPicha: Andrew Kelly/REUTERS

Trump aliendelea kuulaumu uhamiaji haramu kwa kusababisha ghasia za magenge nchini Marekani, akiahidi kuwa atazuia kile alichokiita "uvamizi wa wahalifu wanaoingia nchini humo" iwapo atashinda uchaguzi wa Novemba 5.

Soma pia: Trump na Harris kuendelea na kampeni za mwisho mwisho

Aidha ametoa wito wa adhabu ya kifo kwa mhamiaji yeyote anayemuuwa raia wa Marekani au afisa wa polisi. Naye Kamala Harris, mwenye umri wa miaka 60, alikuwa na siku yenye shughuli nyingi za kampeni katika jimbo la Pennsylvania ambalo ni muhimu kwa matokeo ya uchaguzi wa rais.

Ziara ya Jumapili ilikuwa safari ya 14 ya makamu huyo wa rais jimboni Pennsylvania tangu alipopata tiketi ya kugombea urais baada ya Rais Joe Biden kujiondoa mwezi Julai. Aliwataka Wamarekani kufanya uamuzi ambao hautawafanya wajutie chochote baada ya siku ya uchaguzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW