Trump: Iran imetoa hakikisho la kutounda silaha za nyuklia
31 Mei 2026
Rais wa Marekani Donald Trump amesema amepata hakikisho kutoka kwa Iran kuwa haitotengeneza silaha za nyuklia, wakati kukiwa na ripoti kwamba ametuma pendekezo jipya na lenye masharti makali kwa Tehran.
Mabadiliko yoyote kwenye pendekezo hilo yanaweza kuchelewesha zaidi kufikiwa kwa makubaliano rasmi ya kumaliza vita vya Mashariki ya Katina kufungua njia muhimu ya Mlango Bahari wa Hormuz, baada ya wiki kadhaa za kusaka suluhu licha ya msuguano wa maneno na mapigano ya hapa na pale ya kijeshi.
Vyombo vya habari vya New York Times pamoja na Axios vimeripoti Jumamosi kuwa Trump ametuma pendekezo jipya kwa Iran lenye masharti makali zaidi, ingawa haijabainika ni masharti gani hasa yaliyoongezwa.
Trump amesema vipaumbele vyake katika makubaliano yoyote ni kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia na kufungua tena njia ya Hormuz iliyokuwa imezuiwa.