1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema kuna vitisho vikubwa dhidi yake kutoka Iran

25 Septemba 2024

Maisha ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump yamo hatarini na kitisho kikubwa ni kutoka Iran. Wasimamizi wa kampeini yake wamesema idara ya ujasusi ya Marekani ilitoa onyo kuhusu kitisho hicho.

Donald Trump
Donald Trump Picha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Maisha ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump yamo hatarini na kitisho kikubwa ni kutoka Iran. Wasimamizi wa kampeini yake wamesema idara ya ujasusi ya Marekani ilitoa onyo hilo na kusema kuwa uhalisia wa kitisho hicho kutoka Iran ni mkubwa.

Haikubainika mara moja ikiwa vitisho hivyo vilivyoelezwa na wasimamizi wa kampeini pamoja na Trump mwenyewe ni vipya ama vimeshawahi kuripotiwa awali.

Jaribio la mauaji dhidi ya Trump: FBI yasema Trump alilengwa katika jaribio la mauaji

Katika ujumbe aliouchaoisha kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema, maisha yake yamo hatarini lakini jeshi zima la Marekani linatazama na kusubiri.

Katika taarifa yake,Steven Cheung ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kundi linalohusika na kampeni ya Trump, amesema maafisa wa ujasusi wamebaini kuwa mashambulizi yanayoendelea na yaliyoratibiwa yameongezeka katika muda wa miezi michache iliyopita, na maafisa wa sheria katika mashirika yote wanafanya kazi kuhakikisha Trump analindwa na uchaguzi hauingiliwi kati.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW