1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Lebanon si sehemu ya makubalino ya kusitisha vita

Josephat Charo
9 Aprili 2026

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Lebanon si sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki mbili yaliyoafikiwa, akiliita suala la Lebanon kuwa mzozo tofauti.

Israel imefanya wimbi la mashambulizi nchini Lebanon licha ya usitishwaji vita mashariki ya kati.
Israel imefanya wimbi la mashambulizi nchini Lebanon licha ya usitishwaji vita mashariki ya kati.Picha: Bilal Hussein/AP Photo/picture alliance

Kauli ya Trumo imekuja huku Israel ikifanya wimbi kubwa la mashambulizi dhidi ya Lebanon baada ya makubaliano hayo kutangazwa. Iran kwa upande wake imesema itakomesha usitishaji mapigano kwa upande mmoja ikiwa mashambulizi ya Israel yataendelea dhidi ya Lebanon.

Wizara ya afya ya Lebanon imetangaza idadi ya vifo kutokana na mashambulizi makubwa ya Israeli jana Jumatano kuwa watu 182.

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilisema imekasirishwa na vifo na uharibifu huo mbaya. Kundi la Hezbollah limesema hivi leo limevurumisha maroketi kuelekea kaszini mwa Israel kujibu mashambulizi hayo.

Wakati haya yakiarifiwa, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel iko tayari kurudi vitani  baada ya kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW