Trump: Tuko katika majadiliano mapana na Viongozi wa Cuba
2 Februari 2026
Matangazo
Tamko hili linajiri siku kadhaa baada ya Trump kutishia kuizuwia nchi hiyo kupatamafuta kutoka Venezuela. Hata hivyo rais huyo hakueleza zaidi kuhusu makubaliano anayotarajia kupata kutoka huko.
Hata hivyo wizara ya mambo ya nchi za nje ya Cuba bado haijasema lolote juu ya kauli ya Trump katika taarifa yake iliyoitoa hapo jana Jumapili lakini imesisitiza kuwa kisiwa hicho hakitoi kitisho chochote cha usalama kwa Marekani.
Utawala huo wa Marekani unatoa shinikizo kwa kisiwa hicho tangu Januari 3 ilipoivamia kijeshi Venezuela na kumkamata rais wa taifa hilo Nicolas Maduro ambaye nchi yake ilikuwa mshirika mkubwa wa Cuba na mshirika muhimu pia inayoiuzia mafuta.