1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema Putin anataka kusitisha vita Ukraine

4 Desemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump anaamini kuwa Rais Vladimir Putin wa Urusi anataka kuvimaliza vita nchini Ukraine, licha ya mazungumzo na ujumbe wa Marekani ambayo hayakupata mwafaka huko Moscow.

USA Washington D.C. 2025 | Donald Trump verkündet schwächere Kraftstoffeffizienz-Standards
Picha: Andrew Caballero-reynolds/AFP

Trump ameyasema haya wakati ambapo maafisa hao wa Marekani wanapanga kufanya mazungumzo mengine na mwakilishi mkuu wa Ukraine katika mazungumzo hayo ya kusaka usitishwaji mapigano.

Na sasa baada ya kuulizwa kuhusu mazungumzo hayo, Trump amesema ni mapema mno bado kujua kitakachotokea na akaongeza kuwa mjumbe wake maalum Steve Witkoff na mkwewe Jared Kushner katika mazungumzo yao na Putin, walihisi kuwa ana nia ya kuvimaliza vita hivyo.

Trump vile vile amesema kuwa Ukraine inaliunga mkono kikamilifu pendekezo la Marekani la kusitisha vita. Witkoff na Kushner walifanya mazungumzo marefu na Putin ila wakashindwa kupata mwafaka katika mapigano mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Kremlin ilisema kuwa haikukubaliana na sehemu ya huo mpango wa Marekani wa kusitisha vita licha ya kuwa pendekezo hilo lilijumuisha Ukraine kuachia sehemu kadhaa za eneo la Donbas ambazo bado inazishikilia, miaka minne baada ya uvamizi wa Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW