1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema yuko tayari kuiwekea vikwazo Urusi

15 Septemba 2025

Rais Donald Trump wa Marekani amesema yuko tayari kuiwekea vikwazo zaidi Urusi kutokana na vita vya Ukraine lakini ameyataka mataifa ya Ulaya yachukue hatua sawa ya hiyo ya kuitenga zaidi Urusi.

Marekani Washington D.C. 2025 | Rais Donald Trump akizungumza na waandishi habari mjini Washington
Rais Donald Trump wa Marekani akizungumza na waandishi habari mjini Washington. Picha: Andrew Thomas/NurPhoto/IMAGO

Trump ameaambia waandishi habari mjini Washington kwamba Ulaya bado inanunua mafuta kutoka Urusi na hata vikwazo ilivyoweka dhidi ya Moscow bado havitoshi.

Ameyataka mataifa ya Ulaya kuacha kununua kabisa nishati ya mafuta ya Urusi na kuunganisha nguvu na Marekani kuiwekea vikwazo zaidi vya kiuchumi Urusi.

Trump ametoa matamshi hayo katika wakati washirika wake wa Ulaya wanamshinikiza kuichukulia hatua Urusi kutokana na kujivutavuta kwa Moscow kwenye kumaliza vita vya Ukraine.

Mnamo siku za karibuni Trump amekaririwa akisema amevunjwa moyo na Rais Vladimir Putin wa Urusi kwa kushindwa kwake kuonesha dhamira ya dhati ya kufikia mkataba wa amani na Ukraine licha ya kuahidi kufanya hivyo.