1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump ataka mateka wanaoshikiliwa Gaza waachiwe huru

24 Septemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amelaani hatua zilizochukuliwa na mataifa ya Magharibi kulitambua taifa huru la Palestina.

Marekani 2025 | Rais wa Marekani Donald Trump
Trump amezungumzia vita vya Urusi na Ukraine, mabadiliko ya tabianchi, na uhamiaji haramuPicha: Mandel Ngan/AFP

Akihutubia Jumanne katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Trump amesema nchi zenye nguvu duniani zinapaswa kuangazia juhudi za kuhakikisha mateka wanaoshikiliwa Gaza wanaachiwa huru.

Trump amezungumzia pia vita vya Urusi nchini Ukraine, mabadiliko ya tabianchi, na uhamiaji haramu.

Viongozi wengine waliohutubia Jumanne katika Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa ni pamoja na Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, na Mfalme Abdullah II wa Jordan.

Viongozi hao kwa nyakati tofauti walizungumzia kuhusu matumizi ya silaha, mizozo ya kimataifa, kuongeza misaada ya maendeleo, na kupunguza madeni kwa nchi maskini zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW