Trump ataka Netanyahu apewe msamaha wa rais
12 Novemba 2025
Kulingana na ofisi ya Herzog, Trump ametuma barua kwa Herzog leo akisema kesi dhidi ya Netanyahu ambaye kwa pamoja wamekuwa wakipambana na Iran, ni kesi iliyochochewa kisiasa.
Ofisi hiyo ya rais wa Israel lakini imesema mtu yeyote anayetaka msamaha wa rais ni sharti awasilishe ombi rasmi kwa mujibu wa mwongozo uliopo.
Tump alipofanya ziara Israel mwezi uliopita wa Oktoba, alitoa wito kama huo kwa Herzog. Netanyahu na mkewe Sara katika mojawapo ya kesi hizo wanatuhumiwa kupokea vitu vya thamani ya zaidi ya dola 260,000 kutoka kwa mabilionea waliotaka kufanyiwa hisani za kisiasa.
Katika kesi nyengine mbili, waziri mkuu huyo wa Israel pia anatuhumiwa kujaribu kuvishawishi vyombo viwili vya habari nchini Israel kutoripoti habari mbaya kumhusu.
Netanyahu anakanusha mashtaka hayo na amesema kuwa hana hatia.