1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atangaza kusitisha mapigano kwa wiki mbili nchini Iran

8 Aprili 2026

Tangazo hilo limetolewa chini ya saa mbili kabla ya tarehe ya mwisho aliyoiweka ambayo alidai kuwa ikiwa Iran haitaufungua Mlango bahari wa Hormuz basi ustaarabu mzima nchini Iran ungeangamizwa usiku wa kuamkia leo.

 Washington D.C. 2026 | Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Evan Vucci/REUTERS


Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha mapigano kwa wiki mbili dhidi ya Iran baada ya kupokea pendekezo la kumaliza vita lenye vipengele 10 kutoka Tehran.

Tangazo hilo limetolewa chini ya saa mbili kabla ya tarehe ya mwisho aliyoiweka ambayo alidai kuwa ikiwa Iran haitaufungua Mlango bahari wa Hormuz basi ustaarabu mzima nchini Iran ungeangamizwa usiku wa kuamkia leo.

Katika chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii, Trump amesema kwamba amefikia uamuzi huo baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif na Jenerali Asim Munir, mkuu wa jeshi mwenye nguvu nchini Pakistani.

Pakistan ambayo ni mpatanishi katika mzozo huo imethibitisha kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Israel pia zimekubaliana usitishaji mapigano wa haraka kila mahali, ikiwemo nchini Lebanon.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran,Abbas Araghchi amesema kwamba sasa Mlango Bahari wa Hormuz utafunguliwa kwa wiki mbili lakini kwa ushirikiano na usimamizi wa vikosi vya jeshi la Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW