Trump atangaza ushuru mpya unaozilenga kampuni za dawa
26 Septemba 2025
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza ushuru mpya utakaoanza Oktoba 1, kwa kampuni za dawa, malori makubwa, vifaa vya ukarabati wa majumbani na samani, na kufufua upya vita vyake vya kibiashara duniani.
Katika tangazo lake, Trump amesema bidhaa yoyote ya dawa yenye chapa au zilizo na hati miliki zitatozwa ushuru wa asilimia 100, isipokuwa tu kama kampuni zitajenga viwanda vya uzalishaji dawa ndani ya Marekani.
Malori makubwa kutoka nje yatatozwa ushuru wa asilimia 25, ili kulinda wazalishaji wa ndani. Samani na vifaa vya ukarabati wa nyumba pia vimewekwa kwenye orodha ya ushuru mpya. Kwa mujibu wa Trump, bidhaa hizi zimekuwa zikifurika sokoni kutoka nje, na hatua hiyo inalenga kulinda viwanda vya ndani vya Marekani.
Hatua hizi ni mwendelezo wa vita vya kibiashara vya Trump, na zinaweza kuathiri bei za bidhaa, mahusiano ya kimataifa, na sekta ya afya.