1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atangaza vikosi vya Marekani kuishambulia IS, Nigeria

26 Desemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema vikosi vya Marekani vimefanya mashambulizi makali dhidi ya kundi linalojiita dola la kiislam IS kaskazini magharibi mwa Nigeria. Trump ametishia kwamba watafanya mashambulizi zaidi.

Marekani I Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amesema vikosi vya Marekani vimefanya mashambulizi makali dhidi ya kundi linalojiita dola la kiislam IS kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Akiutumia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amevipongeza vikosi vya Marekani kwa mashambulizi hayo na kuapa kwamba wataendelea kufanya hivyo ikiwa kundi hilo litaendelea kuwaua Wakristo.

Kamandi ya Marekani barani Afrika imesema mashambulizi hayo iliyosema ni kwa ombi la mamlaka ya Nigeria na kwamba yamewaua magaidi wengi.

Nigeria kupitia wizara yake ya mambo ya nje imethibitisha mashambulizi hayo na kusema kwamba yamelenga maeneo sahihi ya magaidi wa kundi hilo.Tukio hili la hivi punde linakuja wakati hali ya ukosefu wa usalama ikiongezeka katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW