1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump atangaza vikwazo 'vikubwa' dhidi ya Urusi

23 Oktoba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vikwazo kwa kampuni mbili kubwa zaidi za mafuta za Urusi.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Allison Robbert/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Akitangaza vikwazo hivyo Trump amesema mazungumzo yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin ya kumaliza vita vya Ukraine 'hayaendi popote.'

Kwa miezi mingi, Trumpamejizuia kuiwekea Urusi vikwazo, lakini uvumilivu wake ulifikia mwisho baada ya mipango ya kukutana na Putin huko Budapest kugonga mwamba.

''Jambo pekee ninaloweza kusema ni kwamba kila ninapozungumza na Vladimir, tunakuwa na mazungumzo mazuri. Na kisha hayaendi popote. Lakini tizama, anapigana vita. Yuko kwenye vita vikali vya pande mbili. Na ndivyo vita vilivyo. Lakini ninaweza kusema muda umewadia. Muda umewadia wa kufikia makubaliano. Watu wengi wanakufa,' amesema Trump'

Umoja wa Ulaya pia ulitangaza vikwazo vipya kuishinikiza Urusi kumaliza vita vyake Ukraine ambavyo vimedumu kwa miaka mitatu na nusu sasa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyamepongeza vikwazo hivyo vipya vya Marekani na Umoja wa Ulaya, akivitaja kuwa ujumbe thabiti na unaohitajika zaidi kuishinikiza Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW