Trump atishia kuiondoa Marekani katika muungano wa NATO
1 Aprili 2026
Matangazo
Trump amesema baadhi ya wanachama wa Jumuiya hiyo wamekataa kutuma meli zao za kivita kusaidia kuufungua Mlango Bahari wa Hormuz.
NATO, inayojumuisha nchi za Ulaya, Marekani na Canada, iliundwa mwaka 1949 kwa lengo la kukabiliana na tishio la mashambulizi ya Umoja wa Kisovieti na kwa miongo kadhaa imekuwa nguzo muhimu ya usalama wa nchi za Magharibi.
Kauli ya Trump imejiri saa chache baada ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, kushindwa kuhakikisha dhamira ya Marekani katika ulinzi wa pamoja wa NATO, hakikisho ambalo ni muhimu kwa muungano huo.
Kwa muda mrefu wataalamu wamekuwa wakionya kuwa kauli zinazoonesha kwamba haiko tayari kuwa pamoja na NATO na kuifanya Urusi kuendelea kuwa kitisho kwa Ulaya.