1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kuiwekea vikwazo Urusi ikikataa mazungumzo ya mani

22 Januari 2025

Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema Jumanne kwamba huenda akaweka vikwazo dhidi ya Urusi iwapo Rais Vladimir Putin hatakubali kufanya mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine.

Marekani | Rais Donald Trump
Rais Donald Trump akimaliza kuzungumza katika mkutano na waandishi habari, ikulu ya Whitr House, Januari 21, 2024.Picha: Carlos Barria/REUTERS

Hata hivyo, hakutoa ufafanuzi juu ya aina ya vikwazo vipya, ingawa tayari Marekani imeiwekea Urusi vikwazo vikali kufuatia uvamizi wake wa Februari 2022.

Trump pia alidokeza kwamba serikali yakeinatafakari suala la kutuma silaha kwa Ukraine, akiongeza maoni yake kwamba Umoja wa Ulaya unapaswa kufanya mengi zaidi kuiunga mkono Ukraine.

Soma pia: Trump asema atakutana 'haraka sana' na Putin.

Alisema wako katika mawasiliano na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, na wanatarajia kuzungumza na Putin hivi karibuni.

Vilevile, Trump alieleza kuwa alimhimiza Rais wa China, Xi Jinping, kutumia ushawishi wake kumaliza vita hivyo, akibainisha kuwa licha ya China kuwa na nguvu kubwa, Xi hajaonyesha juhudi za kutosha kusitisha mgogoro huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW