1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atishia kukatiza msaada kwa Colombia

19 Oktoba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema leo Jumapili kuwa atakatiza ufadhili wa nchi yake kwa Colombia kwa sababu kiongozi wake Gustavo Petro hachukui hatua za kukabiliana na shughuli za dawa za kulevya.

Marekani New York 2025 | Rais wa Columbia kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Rais wa Colombia, Gustavo Petro Picha: Leonardo Munoz/AFP

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, Trump alimtaja Petro kama "mfanyabiashara haramu wa dawa za kulevya anayechukuliwa kuwa wa hadhi ya chini na asiyependwa na watu wengi''.

Amemuonya Petro kuchukuwa hatua dhidi ya shughuli hizo za dawa za kulevya ama Marekani itaingilia kati kwa hatua ambazo hazitakuwa nzuri.

Marekani yaishtumu Colombia kwa kutoshirikiana nayo kukabiliana na dawa za kulevya

Ujumbe huo uliochapishwa wakati ambapo Trump alikuwa katika mapumziko kwenye eneo lake la Mar-a-Lago huko

Florida, ni ishara ya hivi punde zaidi ya msuguano kati ya Marekani na mmoja wa washirika wake wa karibu katika Amerika ya Kusini.

Mnamo mwezi Septemba, serikali ya Marekani iliishutumu Colombia kwa kukosa kushirikiana nayo katika vita dhidi ya madawa ya kulevya, ingawa wakati huo ilitoa nafuu ya vikwazo ambavyo vingesababisha kupunguzwa kwa misaada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW