1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Trump atishia kushambulia nishati ya umeme ya Iran

22 Machi 2026

Rais wa Marekani Donald Trump, ameonya kwamba nchi yake itaishambulia na kuiharibu kabisa miundombinu ya nishati ya umeme iwapo Jamhuri hiyo ya kiislamu haitoufungua mlango bahari wa Hormuz katika muda wa saa 48.

USA Washington D.C. 2026 | Donald Trump
Trump atishia kushambulia nishati ya umeme wa Iran iwapo Tehran haitofungua mlango Bahari wa Hormuz ndani ya saa 48Picha: Nathan Howard/REUTERS

Hayo yanajiri wakati makombora mawili ya Iran, yakivurumishwa katika miji miwili ya Israel iliyoko karibu na kituo kikuu cha utafiti wa nyuklia cha Tel Aviv na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku majengo yakiharibiwa vibaya.

Matukio hayo yanaonyesha kuwa vita hivyo vya Mashariki ya Kati, vinavyoingia wiki yake ya nne, vinaelekea hatarini. Hii leo Jumapili Vin'gora vilisikika Israel vikitoa onyo la shambulio kabla ya miji hiyo miwili ya kusini ya Dimona na Arad kushambuliwa.

Hapo jana Rais Donald Trump aliionya Iran kwamba anaipa saa 48 ya kuufungua mlango bahari huo wa Hormuza au mitambo yake ya umeme ishambuliwe. Hata hivyo Iran imeonya kuwa shambulio lolote dhidi ya miundombinu yake litajibiwa kwa mashambulizi makali pia dhidi ya miundombinu ya Israel na Marekani katika kanda hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW