1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atishia kuzisimamisha shughuli za serikali

Saumu Mwasimba
12 Desemba 2018

Trump ameingia kwenye malumbano makali ya viongozi wawili wa juu wa Democrats juu ya ujenzi wa ukuta wa mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Washington Chuck Schumer  bei Trump Gespräche Haushaltssperre
Trump akilumbana na Chuck Schumer kiongozi wa seneti wa DemocratsPicha: picture-alliance/CNP/M. Reynolds

Rais wa Marekani Doland Trump amepambana hadharani kwa kutupiana maneno na wabunge wawili wa ngazi ya juu wa chama cha Democrat katika ikulu hapo jana. Mvutano huo umesababishwa na suala la gharama za ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na mpaka wa Mexico.

Rais Trump amefikia umbali wa kusema atazisimamisha shughuli zote za serikali ikiwa fikra yake ya kuulinda mpaka wa Marekani na Mexico itazuiwa na wanademocrats.

''Ikiwa hatutopata tunachokitaka kwa njia moja au nyingine ikiwa ni kupitia wewe au jeshi au kupitia  kitu kingine chochote unachotaka kukitaja.mimi nitazifunga shughuli zote za serikali.Ninajivunia kusimamisha shughuli za serikali kwa ajili ya usalama wa mpaka wetu''

Malumbano hayo yamejitokeza katika ikulu wa White House mbele ya kamera za waandishi habari yakimuhusisha pia spika wa bunge kutoka upande wa Democrats Nancy Pelosi na makamu wa rais Mike Pence aliyekuwa amekaa kando ya rais Trump. Hivi sasa chama cha rais Trump cha Republican bado kinayadhibiti mabaraza yote mawili baraza la seneti na bunge mpaka mwezi ujao wa Januari. Ungaaji mkono wa chama cha Democratic lakini unahitajika ili kuidhinisha sheria ya matumizi ya aina yoyote ya serikali.

Picha: Reuters/K. Lamarque

Trump amelitaka bunge liidhinishe dolla bilioni 5 kwa ajili ya ulinzi wa mpaka na Mexico lakini viongozi wawili wa Democrats kiongozi wa  seneti Schumer pamoja na spika wa bunge Pelosi wameridhia kutoa dolla bilioni 1.3 tu. Kwa kauli aliyoitowa rais Trump inamaanisha ikiwa hakuna mwafaka utakaopatikana kati yake na Democrats rais huyo huenda akayafunga mashirika yanayohusika na suala hilo hilo la usalama wa mipaka-kwamaneno mengine shughuli za wizara ya usalama wa ndani zitasimamishwa.wizara za mambo ya nje,biashara na kilimo zote zitalengwa.

Mkutano kati ya Trump,Pelosi na Schumer ulikuwa wa kwanza tangu Democrats wanyakue ushindi na kulidhibiti bunge katika uchaguzi wa katikati ya muhula uliofanyika Novemba. Lakini mbali na mvutano huo kuhusu mpaka wa Mexico Trump pia ameshikilia msimamo wake wa kumuunga mkono mrithi wa ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman katika kisa cha kuuliwa mwandishi habari Jamal Khashoggi licha ya tathmini ya shirika la ujasusi la cia kwamba mwanamfalme huyo ndi aliyetoa maagizo ya kuuliwa Khashoggi na licha pia ya miito ya maneseta wa Marekani kumtaka alaani kitendo cha mwanamfalme.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Iddi Ssessanga