1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atuma pendekezo la mpango wa amani kwa Iran

25 Machi 2026

Rais wa Marekani Donald Trump ametuma pendekezo la mpango wa amani kwa Iran wakati akitoa matumaini ya kukomesha vita vilivyodumu kwa karibu mwezi mmoja.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump ametuma pendekezo la mpango wa amani kwa Iran wakati akitoa matumaini ya kukomesha vitaPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/dpa/picture alliance

Gazeti la New York Times, likiwanukuu maafisa ambao hawakutajwa majina, lilisema Marekani imetuma pendekezo la mpango wa vifungu 15 kwa Iran kupitia kwa Pakistan. Televisheni ya Israel ya Channel 12 ilisema Trump miongoni mwa mengine, anapendekeza kusitisha mapigano kwa mwezi mmoja ambapo pande hizo zitajadili pendekezo ambalo litajumuisha Iran kukabidhi madini ya urani yaliyorutubishwa na kupiga marufuku urutubishaji zaidi.

Akizungumza na waandishi Habari katika Ikulu ya White House, Trump alisema Marekani "inafanya mazungumzo hivi sasa" na Iran -- ambayo haijathibitisha kuwepo kwa mazungumzo yoyote rasmi. Licha ya matumaini ya Trump ya diplomasia, jarida la Wall Street limeripoti kwamba Marekani inapanga kuwapeleka Mashariki ya Kati wanajeshi 3,000 kutoka Kikosi cha 82 cha Wanajeshi wa Anga.

Hayo yanajiri wakati Tehran ikitangaza kwamba itaruhusu meli za mafuta "zisizohusika na vita" kupita katika Mlango-Bahari muhimu wa Hormuz.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW