1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akosoa viongozi wa California kushindwa kudhibiti moto

Sylvia Mwehozi
12 Januari 2025

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amewashutumu viongozi wa California kwa kushindwa kushughulikia janga la moto mkali unaoendelea kuiteketeza Los Angeles.

Marekani| Los Angeles | moto
Afisa wa mima moto akikabiliana na moto Los AngelesPicha: DW

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amewashutumu viongozi wa California kwa kushindwa kushughulikia janga la moto mkali unaoendelea kuiteketeza Los Angeles.

Kupitia mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema moto huo, ni moja ya majanga makubwa katika historia ya Marekani na kuwakosoa wanasiasa aliowataja kutokuwa na uwezo, kwa namna wanavyo shughulikia kadhia hiyo.

Kasi na ukali wa moto huo, umetoa changamoto kwa miundombinu ya kuzima moto na kuzua maswali pamoja na ukosoaji juu ya utayari wa serikali kukabiliana na hali hiyo. Hadi sasa moto huo umesababisha vifo vya watu 16, kuwahamisha watu 150,000 na kuharibu zaidi ya miundombinu 12,000 kulingana na maafisa wa serikali.

Licha ya juhudi za maafisa wa zima moto, ikiwemo kuuzima moto kutokea angani, moto huo wa nyika katika kitongoji cha Palisades umeendelea kusambaa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW