SiasaMarekani
Trump awalaumu "mrengo wa kushoto" mauaji ya Kirk
11 Septemba 2025
Matangazo
Trump aliandika kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba wanasiasa wa mrengo mkali wa kushoto "wamekuwa wakiwalinganisha Wamarekani wazuri kama Charlie na Manazi na ndio chanzo cha mauaji na ugaidi ndani ya nchi."
Kirk, ambaye alikuwa muasisi na kiongozi mwenza wa kundi la vijana lililosaidia kampeni ya kumrejesha madarakani Trump, alipigwa risasi na kuuawa siku ya Jumatano (Septemba 10) akiwa kwenye mkutano katika Chuo Kikuu cha Uttah Valley.
Picha ya video inamuonesha Kirk akianguka jukwaani alipokuwa akizungumza baada ya mlio wa risasi kusikika.
Wapelelezi wanaamini hayo yalikuwa mauaji ya kupanga na kwamba muuaji alikuwa amekaa kwenye paa la chuo hicho.