1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump awataka washirika wake "wajitokeze" kusaidia vita

20 Machi 2026

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaka Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi "kujitokeza" wakati akiwashinikiza wandani wake kusaidia katika vita dhidi ya Iran na ongezeko la bei ya mafuta.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Waziri Mkuu wa Japan sanae Takaichi
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Waziri Mkuu wa Japan sanae TakaichiPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Trump ameitetea operesheni ya Marekani dhidi ya Iraniliyowashangaza washirika wake na ametumia mkutano wake na Takaichi kuwashinikiza washirika hao wa Marekani barani Asia na Ulaya.

Rais huyo ametoa wito wa meli zaidi kutumwa na mataifamengine katika mlango bahari wa Hormuz uliofungwa na Iran, ili kusindikiza meli za mafuta kuvuka.

Trump awali alikuwa amesema kuwa Marekani haihitaji usaidizi wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Trump, Takaichi amesema amemueleza Trump msaada ambao katiba ya Japan inaikubalia nchi hiyo kuutoa na kutotoa katika mlango huo bahari wa Hormuz.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW