1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump awaza mbinu za kuendelea kuupinga ushindi wa Biden

Iddi Ssessanga Mhariri: Zainab Aziz
8 Novemba 2020

Rais Donald Trump hakubali kuwa ameshindwa anakabiliwa na ukweli mgumu kwamba sasa Joe Biden wa chama cha Demokratik ameshinda kinyang'anyiro cha kuingia ikulu ya Marekani:

USA I Präsidentschaftswahl 2020 I Joe Biden - Donald Trump
Picha: Chris Kleponis/Captital Pictures/picture alliance

Bada ya karibu siku nne za kuhesabu kura kulikompa ushindi Biden mnamo siku ya Jumamosi, Trump alikuwa bado anasisitiza kwamba kinyang'anyiro hicho hakijamalizika. Ametoa madai yasio na msingi kuhusu udanganyifu, ameahidi hatua za kisheria na kuchapisha ujumbe wa Twitter anamodai kwamba ameshinda uchaguzi huu kwa tofauti kubwa. Trump bado anatafakari njia za kuendeleza mapambano. 

Hamna tamaa ya Trump kukubali kushindwa

Kulingana na watu walio karibu naye, Trump hatarajiwi kamwe kukubali rasmi kushindwa, lakini anaweza kuondoka ikulu huku akilalamika mwishoni mwa muhula wake. Juhudi zake zinazoendelea kuuonesha uchaguzi huo kuwa usiyo wa haki, zinatazamwa kama zenye lengo la kutuliza nafsi iliyojeruhiwa, na kuwaonesha wafuasi wake watiifu kwamba bado anapambana. Hilo linaweza kuwa muhimu kuwabakisha na shauku ya kile kinachofuata.

Soma zaidi:Ushindi wa Joe Biden: Huruma imeshinda urais

Mshauri wake wa masuala ya kiuchumi Larry Kudlow, amesema rais Trump ananuwia kuendelea kupigania matokeo ya uchaguzi, ambayo yanaendelea kuhesabiwa katika majimbo muhimu. Akizungumza na waandishi habari nje ya ikulu mano siku ya Ijumaa, Kudlow alikataa kusema iwapo Trump atakubali kuwa ameshindwa iwapo Biden angevuka idadi ya wajumbe 270 wanaohitajika kwa mgombea kutangazwa mshindi.

Rais mteule wa Marekani Joe BidenPicha: Jim Watson/AFP/Getty Images

Rafiki yake TNew Yorkrump asema ana mashaka

Rafiki wa muda mrefu wa Trump Roger Stone, ambaye kifungo chake cha muda mrefu kilipunguzwa na Trump mwezi Julai, amesema ana mashaka iwapo Trump anaweza kukubali kushindwa. Stone amesema matokeo ya hilo ni kwamba Biden atakuwa na kiwingu juu ya urais wake, ambapo nusu ya watu nchini wakiamini kwamba alichaguliwa kinyume cha sheria.

Washirika wanasema iwapo Trump anataka kuanzisha himaya ya vyombo vya habari katika miaka ijayo, ana msumukumo wa kuendeleza sarakasi hizo. Vivyo hivyo, ikiwa ananuwia kuacha milango wazi kwa ajili ya uwezekano wa kurudi mwaka 2024 - atakuwa mwaka mmoja zaidi ya umri wa sasawa Biden.

Angalia:

Wafuasi wa Trump waandamana Biden akiongoza uchaguzi

01:01

This browser does not support the video element.

Wapo wengi miongoni mwa watu wake wa ndani wanaomhimiza kuendelea na mapambano, akiwemo wakili wake, Rudy Guiliani. Meya huyo wa zamani wa mji wa New York amekuwa akiahidi kumpa rais ushahidi wa udanganyifu wa kura lakini ametoa kidogo sana, ikiwemo wakati wa mkutano wa waandishi habari alioufanya jana Jumamosi mjini Philadelphia. Watoto wakumbwa wa kiume wa Trump, Donald Jr. na Eric, pia wamemhimiza baba yao kuendelea na mapambano na kuwataka Warepublican kusimama nao. Hata hivyo washirika wengine na maafisa wa White House, wamemhimiza Trump kubadili toni na kurahishisha mchakato wakukabidhi madaraka kwa amani. Wamemsisitizia kwamba historia itahukumu vikali hatua zozote anazozichukuwa ambazo zinaonekana kama zinamdhoofisha mrithi wake. Na wamemshauri kutoa hotuba katika wiki zijazo akiahidi kusaidia kipindi cha mpito.

Chanzo:AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW