1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais mteule wa Marekani Trump azungumza na Rais Putin

11 Novemba 2024

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amezungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin na kumtolea wito wa kutovízidisha vita nchini Ukraine, gazeti la Washington Post limearifu siku ya Jumapili.

Trump na Putin
Rais mteule wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Wakuu hawa wamearifiwa kuzungumza masuala kadha wa kadhaPicha: ZDF

Trump alizungumza kwa simu na Putin kutokea kwenye makazi yake ya Mar-a-Lago huko Florida siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kushinda uchaguzi.

Hata hivyo, wawakilishi wa Trump hawakutaka kuzungumzia suala hilo walipoulizwa na shirika la habari la AFP.

Gazeti hilo, limenukuu vyanzo viwili vyenye uelewa na mazungumzo hayo ambao hawakutaka kutambulishwa kwamba Trump alimkumbusha Putin juu ya ukubwa wa jeshi la Marekani barani Ulaya.

Trump pia alielezea nia ya mazungumzo ya zaidi kuhusu "suluhisho la vita vya Ukraine hivi karibuni."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW