1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump hajalipa kodi ya mapato kwa miaka mingi

Sekione Kitojo
28 Septemba 2020

Gazeti  la New York Times limeripua bomu na kufichua kwamba rais Donald Trump alilipa kiasi cha dola 750 tu za kodi ya mapato wakati wanasiasa hao wakijitayarisha kuingia katika mdahalo Jumanne .

USA PK Donald Trump
Donald TrumpPicha: Brendan Smialowski/AFP/Getty Images

Trump  amefanyakazi  kwa  miongo  kadhaa  akijenga taswira yake kama  mfanyabiashara  mwenye  mafanikio  makubwa, na  hata kuchagua  kujipachika  jina  la  'tajiri kigogo' .

Lakini  gazeti  la  New York Times lilifichua  kwamba  alilipa kiasi  cha  dola  750 katika kodi ya mapato  katika  mwaka  2016, mwaka  ambao  alishinda  uchaguzi wa  rais, na  mwaka  2017, mwaka  wake  wa  kwanza  akiwa madarakani. Katika  miaka  10 kati ya miaka  15 iliyotanguliwa 2016, hakulipa kodi ya yote, kwa kiasi kikubwa  aliripoti  kupoteza  fedha nyingi  kuliko  alizopata,kwa  mujibu wa  gazeti  hilo  la  New York Times, ambalo  lilipata  data za miaka  kadhaa  za  marejesho  ya kodi  ambazo  rais  alipambana  kuzificha.

Mgombea wa chama cha Democratic Joe BidenPicha: MSNBC/Zuma/picture-alliance

Hali  hiyo  inakuja   katika  wakati  mgumu kwa  Trump, ambae kampeni  yake  ya  chama  cha  Republican  inayumba yumba kuweza  kujitoa ukosoaji wa jinsi  rais  anavyoshughulikia  janga  la virusi  vya  corona. Taarifa  hiyo  inampa Joe Biden  njia  nyepesi ya kumshambulia wakati  wakiingia  katika  mdahalo wa  kampeni kesho  Jumanne.

Na wakati upigaji  kura wa  mapema  tayari unaendelea  katika  baadhi  ya  majimbo na  siku  ya  uchaguzi ikiwa ni  baada  ya  mwezi  mmoja tu, Trump inaelekea  muda unamwendea mbio  kuweza  kurejesha  mwendo  wa  kampeni  yake katika  utulivu.

Taarifa za uongo

Kuhusu taarifa  hiyo  ya  gazeti  la  New York Times Trump  alisema, hiyo ni  taarifa  ya  uongo.

Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP/dpa/picture-alliance

"Hii ni  habari ya uongo, ni uongo mtupu, imetengenezwa. Tutafanya taarifa  kama  hizo , mngeniuliza  maswali  kama  hayo, miaka  minne iliyopita kuhalalisha  hili  na tukazungumzia  hilo. Ni taarifa ya uongo kabisa.

Hapana, kwa hakika  nalipa kodi, na  utaona  kwamba  mara marejesho yangu yatakapofanyika, yanafanyiwa uhakiki wa chini, zimekuwa  zikifanyiwa uhakiki wa chini  kwa  muda  mrefu, idara inayohusika na  kodi  hainitendei  vizuri. Wananifanyia  kama hafla ya kunywa  chai."

Donald Trump  anahitaji  uchaguzi  huu  uwe  kuhusu  Joe Biden, kama  anavyoeleza  mshauri  wa  muda  mrefu wa  chama  cha Republican  Alex Conant anavyosema.  Lakini  hili  linamwelekea moja kwa moja  Trump  na  kuchunguza  tabia  yake  na mkanganyiko  uliopo  wakati tukiingia  katika  usiku muhimu  sana  wa kampeni, ambapo utafanyika  mdahalo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW