1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Hatutakubali Iran ´itucheze shere´

18 Aprili 2026

Rais Donald Trump wa Marekani ameionya Iran "kuichezea akili" Washington kwa kupinduapindua uamuzi juu ya Mlango Bahari wa Hormuz baada ya Tehran kutangaza kuufunga tena ujia huo muhimu wa bahari.

USA Washington D.C. 2026 | Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Salwan Georges/UPI Photo/IMAGO

Akizungumza wakati wa halfa moja iliyofanyika ikulu ya White House mjini Washington, Trump amesema linapohusika suala la Mlango huo Marekani haitokubali kuchezewa shere na Iran, kama dola hiyo ya Uajemi ilivyofanya kwa miaka mingi. 

Awali Kamandi Kuu ya Jeshi la Iran ilitangaza kurejesha vizuizi vyote kwenye Mlango Bahari wa Hormuz, baada ya hapo jana Ijumaa kusema kuwa imeufungua na kuruhusu meli nyingi zaidi kupita.

Tehran imesema imechukua uamuzi huo baada ya Washington kukiuka ahadi ya kufunguliwa kikamilifu mlango bahari huo ikiwa ni pamoja na kusitisha mzingiro wa kijeshi iliyouweka dhidi ya bandari za Iran.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW