1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kufanya mkutano wake wa kwanza tangu jaribio la kumuua

21 Agosti 2024

Donald Trump hii leo atafanya mkutano wa kampeni katika huko North Carolina. Huu ndio utakaokuwa mkutano wa kwanza Trump kuufanya nje tangu alipoponea jaribio la kumuua katika mkutano kama huo mwezi mmoja uliopita.

Trump na Elon Musk X.com Space
Mgombea urais wa chama cha Republican na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akizungumza wakati akishiriki katika mahojiano na bilionea mjasiriamali Elon Musk kwenye mtandao wa kijamii wa X,Picha: Margo Martin via REUTERS

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kwamba usalama unaimarishwa kuelekea mkutano huo, ikiwemo kioo kisichopenya risasi kuzungushwa katika jukwaa atakalotumia mgombea huyo wa urais wa chama cha Republican. Shirika la Secret Service linalotoa huduma kwa wanasiasa mashuhuri nchini Marekani lilikuwa limempendekezea Trumpasifanye mikutano ya nje, baada ya lile tukio la Pennsylvania ambapo mtu aliyejihami kwa bunduki alimfyatulia risasi na kumjeruhi kwenye sikio lake la kulia. Lakini Trump mwenyewe amesema kwamba anataka kuanza tena kufanya mikutano ya nje.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW