1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump kufika tena mahakamani

13 Juni 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anapanda kizimbani kwenye mahakama moja huko mjini Miami kujibu mashtaka ya kuhifadhi kinyume cha sheria nyaraka za siri za serikali wakati alipoondoka madarakani mwaka 2021.

Donald Trump akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Miami,  Juni 12, 2023 tayari kwenda mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Donald Trump anakabiliwa na mashtaka ambayo ni pamoja na kuwa na nyaraka za usalama wa taifa kinyume cha sheria, alizozichukua baada ya kuondoka mamlakani na kutoa taarifa za uongo.Picha: Win McNamee/Getty Images

Waendesha mashtaka wanasema mwanasiasa huyo pia litowa taarifa za uwongo kwa maafisa wa polisi. Atafika kwenye viunga vya mahakama ya shirikisho ya mji wa Miami akikabiliwa na jumla ya mashtaka 37 yote ikiwa ni kuhusu madai kwamba alivunja sheria kwa kukusanya na kuondoka na nyaraka chungunzima za siri alipoachia madaraka Januari mwaka 2021.

Waendesha mashtaka wanasema nyaraka hizo zinajumuisha zile siri ya kiwango cha juu ikiwemo taarifa za silaha za nyuklia za Marekani na mikakati ya kiusalama ya Washington ya kujibu hujuma yoyote kutoka nje. Duru zinasema atakuwa pamoja na mshtakiwa mwenzake Walt Nauta ambao wote wamejumuishwa kwenye kesi hiyo.