1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiMarekani

Trump kuhudhuria kesi dhidi yake katika Mahakama, Washington

9 Januari 2024

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anatarajiwa hii leo kuhudhuria kesi yake katika mahakama ya shirikisho.

Donald Trump alipohudhuria kesi dhidi yake mjini New York
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akihudhuria kesi dhidi yake mjini New York: 07.12.2023Picha: Andrea Renault/ZUMA/picture alliance

Trump atatetea hoja yake mpya ya kwamba, kama rais wa zamani hapaswi kushtakiwa kwa tuhuma za kutaka kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.  

Hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa Machi 4 mwaka huu mjini Washington katika chumba cha mahakama kilicho karibu na jengo la Bunge lililovamiwa na wafuasi wa Trump Januari 6 mwaka 2021.  

Mawakili wa Trump wanajaribu kufuta mashtaka dhidi ya mteja wao kwa hoja mpya kwamba rais wa zamani ana "kinga kamili" na hawezi kufunguliwa mashtaka yeyote kutokana na hatua zake akiwa katika Ikulu ya White House.