1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kukamatwa Jumanne

1 Aprili 2023

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, atakamatwa rasmi na kufikishwa kizimbani Jumanne wiki ijayo kutokana na mashtaka ya jinai dhidi yake.

USA | frühere US-Präsident Donald Trump veranstaltet eine Wahlkampfveranstaltung in Waco, Texas
Picha: Nathan Howard/AP Photo/picture alliance

Haya ni kwa mujibu wa maafisa wa mahakama, hili likiwa tangazo la kihistoria kwa rais wa zamani nchini humo kufikishwa mahakamani.

Wakati mahakama ya Manhattan ilipothibitisha muda huo hapo jana, barabara nje ya mahakama hiyo zilikuwa zimetulia baada ya maandamano yaliyoshuhudiwa mapema wiki iliyopita lakini umati mkubwa wa wanahabari na polisi ulishuhudiwa.

Soma zaidi:Trump kushtakiwa kufuatia malipo kwa Stormy Daniels

Katika mahojiano ya televisheni hapo jana, wakili wa Trump, Joseph Tacopina, alisema atapinga vikali uhalali wa kisheria wa uamuzi wa jopo la mahakama hiyo wa kumshtaki rasmi Trump.

Kupitia mitandao ya kijamii, Trump ameeleeza hasira yake na kulalamika kuwa jaji anayetarajiwa kushughulikia kesi hiyo, Juan Manuel Merchan, anamchukia.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW