1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kukutana na mawaziri kujadili kuhusu vita vya Iran

27 Mei 2026

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na Baraza lake la Mawaziri leo Jumatano wakati mazungumzo ya kumaliza vita na Iran yakiwa bado hayajakamilika.

Marekani Washington D.C. 2025 | Rais Donald Trump akiwa nje ya Ikulu ya White House
Rais Donald Trump akiwa nje ya Ikulu ya White HousePicha: CNP/ADM/Capital Pictures/picture alliance

Trump amesema makubaliano yako karibu, yakilenga kufungua Mlango-Bahari wa Hormuz,  kuongeza muda wa usitishaji mapigano, na kupunguza uwezo wa nyuklia wa Iran.

Lakini mpango huo unakosolewa, hata na baadhi ya wabunge wa chama chake cha Republican, wanaosema masharti yake yanaweza kuonekana kuisaidia Tehran. Iran huenda ikakubali kuachia akiba yake ya uranium iliyorutubishwa kwa kiwango cha juu, kwa kulegezewa vikwazo, lakini maelezo bado yatajadiliwa kwa siku 60.

Mazungumzo pia yamevurugwa na mashambulizi ya Marekani kusini mwa Iran, huku Tehran ikiyaita hatua yenye "nia mbaya.” Suala la Lebanon na Hezbollah bado halijatatuliwa, na Israel imesema inaongeza operesheni zake.

Trump pia anazitaka nchi kama Saudi Arabia, Qatar na Pakistan zijiunge na makubaliano ya Abraham, jambo ambalo linaonekana kuwa gumu kisiasa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW