1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Trump kukutana na kiongozi wa upinzani wa Venezuela

13 Januari 2026

Marekani imesema mwanasiasa wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado, atakutana na Rais Donald Trump, wakati shinikizo likiongezeka kwa uongozi wa mpito mjini Caracas kuharakisha kuwaachilia wafungwa wa kisiasa.

Venezuela | Barinas 2024 | Maria Corina Machado
Mwanasiasa wa upinzani wa Venezuela Maria Corina MachadoPicha: Juan Barreto/AFP

Afisa wa serikali ya Marekani ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mkutano huo utafanyika siku ya Alhamisi katika Ikulu ya White House.

Machado amekuwa akitengwa na Washington tangu majeshi ya Marekani yalipomkamata kiongozi wa muda mrefu Nicolas Maduro tarehe 3 Januari, hatua iliyofuatwa na utawala wa Trump kutangaza kuisimamia Venezuela.

Kwa kumwacha pembeni Machado na mshirika wake Edmundo Gonzalez Urrutia, Trump amekuwa akifanya kazi na rais wa muda Delcy Rodriguez, aliyeachwa madarakani pamoja na washirika wa karibu wa Maduro.

Trump amemwonya Rodriguez kufuata maelekezo ya Marekani — hasa kuhusu kuruhusu upatikanaji wa akiba kubwa ya mafuta ya nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Wakati huohuo, Venezuela imetangaza kuwaachilia huru watu wengine 116 waliokuwa wamefungwa chini ya utawala wa Maduro — wengi wao kwa kushiriki maandamano baada ya uchaguzi wa mwaka 2024 uliogubikwa na utata.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW