Trump kukutana na Ngueso kuijadili Libya
27 Desemba 2016Matangazo
Msemaji wa Nguesso, Thierry Moungalla, amethibitisha taarifa hiyo kupitia mtandao wa Twitter. Wawakilishi wa Trump, anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake Januari 20, hawakuwa tayari kuthibitisha mara moja juu ya kuwepo kwa mkutano huo. Libya imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia pande mbili za kiserikali nchini humo kuhasimiana huku makundi mengine yaliyo na silaha nayo pia yakipambana kuwania madaraka. Mapema mwezi huu, Umoja wa Mataifa ulielezea juu ya mgogoro wa kibinadamu nchini Libya, ambao unazidi kuyafanya mapambano dhidi ya wahamiaji haramu kuwa magumu.