1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kukutana na viongozi wa Rwanda na Kongo Alhamis

2 Desemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Alhamisi hii ili kusaini makubaliano ya amani, Ikulu ya White House imesema.

Marekani Washington D.C. 2025 | Marco Rubio anaongoza mazungumzo ya makubaliano ya amani kati ya Kongo na Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (katikati) katika hafla ya kusaini makubaliano ya amani na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Thérèse Kayikwamba Wagner (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe (kushoto) katika Wizara ya Mambo ya Nje mjini Washington, DC, tarehe 27 Juni 2025.Picha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Mkutano huo unatarajiwa kuboresha makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani mwezi Juni na kutiwa saini na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili, pamoja na mpango mkakati wa  kiuchumi ulioafikiwa mwezi Novemba. Wakati hatua hiyo ikitarajiwa kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda lilifanya mashambulizi ya kushtukiza mashariki mwa Kongo mwaka huu, likiteka miji mikuu miwili ya eneo hilo na kuzua hofu ya vita vikubwa zaidi.