1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump kumteua Huckabee kuwa balozi wa nchini Israel

13 Novemba 2024

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametangaza kumteua Mike Huckabee kuwa balozi wa taifa hilo nchini Israel.

Mrepublican, Mike Huckabee
Mike Huckabee, kiongozi wa kiimani aleyegeukia siasa, katika picha iliyopigwa mwaka 2016 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habariPicha: APImages

Trump amemtaja Huckabee kama mtumishi makini wa umma, gavana na kiongozi wa kiimani kwa miaka mingi akisema anaipenda Israel na waru wa Israel pia wanampenda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar alipongeza uteuzi huo wa Huckabee ambaye aliwahi kusema hakuna kitu kama uvamizi, linapokuja suala la maeneo ya Kipalestina.

Huckabee mwenye miaka 69, aliwahi kuwania nafasi ya kugombea urais mara mbili katika chama chake cha Republican na amekuwa na misimamo mikali dhidi ya haki za wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW