1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kuongoza ibada ya kumbukumbu ya Charlie Kirk

21 Septemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump na maafisa waandamizi katika utawala wake akiwemo makamu wa rais JD Vance, leo wataongoza Ibada ya kumbukumbu kwa ajili ya mwanaharakati wa mrengo wa kulia Charlie Kirk.

Marekani Phoenix 2025 | Kumbukumbu ya Charlie Kirk mbele ya Makao Makuu ya asasi yake ya Turning Point USA
Kirk, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Turning Point USA, alipigwa risasi na kuuawa mnamo Septemba 10Picha: Joe Raedle/Getty Images/AFP

Rais wa Marekani Donald Trump na maafisa waandamizi katika utawala wake akiwemo makamu wa rais JD Vance, waziri wa mambo ya nje Marco Rubio, leo wataongoza Ibada ya kumbukumbu kwa ajili ya mwanaharakati wa mrengo wa kulia Charlie Kirk aliyeuawa kwa kupigwa risasi wiki iliyopita. Kirk, aliyekuwa na umri wa miaka 31, alipigwa risasi shingoni mnamo Septemba 10 wakati akizungumza katika Chuo Kikuu cha Utah, kama sehemu ya mfululizo wa mijadala yake maarufu ya umma. Mamlaka zilimkamata mshukiwa wa tukio hilo baada ya msako wa takribani saa 33, huku waendesha mashitaka wakitaka hukumu ya kifo katika kesi hiyo. Mauaji ya mwanaharakati huyo kijana mhafidhina na mwanzilishi wa kampeni ya vijana ya mrengo wa kulia ya Turning Point Marekani, yamezidisha migawanyiko ya kisiasa nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW