1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Makubaliano ya Greenland yamefurahiwa na kila mmoja

22 Januari 2026

Rais wa Marekani donald Trump amesema kuwa amefikia makubaliano ya mkakati unaomridhisha kuhusu Greenland.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte
Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte (kushoto)Picha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Trump ameyasema hayo wakati ambapo pia amedai kuwa hatotumia nguvu kukichukua kisiwa cha Greenland na pia kudai kuwa hatoziwekea tena ushuru bidhaa za mataifa nane ya Ulaya yaliyokuwa yanaupinga mpango wake wa kuitwaa Greenland.

Akizungumza na kituo cha habari cha Marekani CNBC,Trump amesema makubaliano hayo ni ya muda mrefu na kila mmoja ameyafurahia ila hakutoa taarifa zaidi na hakusema pia iwapo hiyo inamaanisha kuwa Marekani itakuwa na udhibiti wa kisiwa hicho cha eneo la Arctic.

Tahadhari ya matumaini ya mapema

Trump ameyasema yote hayo baada ya mkutano huko Davos na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte ambaye kupitia msemaji wake, ameyathibitisha hayo aliyoyasema Trump.

Trump akizungumza katika Jukwaa la Kiuchumi Duniani, mjini DavosPicha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Lakini waziri wa fedha wa Ujerumani Lars Klingbeil ameonya dhidi ya kuwepo kwa matumaini ya mapema kutokana na hiyo kauli ya Trump kuwa sasa hatoziwekea tena bidhaa za Ulaya ushuru.

Vitisho vya Trump vilikuwa vimezusha mmojawapo wa mizozo mikubwa zaidi katika eneo la transatlantic kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa, akisema kwamba anaweza kuisambaratisha NATO.

Denmark yakaribisha nguvu kutotumiwa

Lakini sasa Waziri Mkuu wa Denmark Dick Schoof amesema kuwa Marekani na Ulaya kwa sasa ziko katika njia ya kusuluhisha tofauti zao.

Waziri Mkuu wa Denmark Dick SchoofPicha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images

Waziri wa mambo ya kigeni wa Denmark Lars Lokke Rasmussen naye ameikaribisha hatua ya Trump kutotumia nguvu katika azma yake ya kutaka kuichukua Greenland ila ameonya kuwa rais huyo wa Marekani ana malengo ambayo hawawezi kuyakubali.

Kabla Trump kutangaza mabadiliko hayo ya kimsimamo kuhusu Greenland, serikali ya kisiwa hicho ilikuwa imewapa ushauri raia wake kuhusiana na hatua za kuchukua endapo kutakuwa na "mzozo" nchini humo.

Vyanzo: AFP/DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW