1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump: Marekani itazimiliki meli za mafuta ilizozikamata

23 Desemba 2025

Rais Donald Trump wa Marekani amesema meli za mafuta ambazo aliamuru zikamatwe nje kidogo mwa pwani ya Venezuela zitabakia kuwa mali ya Marekani.

Venezuela | Meli ya mafuta
Venezuela imekosoa vitendo vya ukamataji meli za mafuta vinavyofanywa na Marekani.Picha: DW

Akijibu maswali ya waandishi habari mjini Washington, Trump amesema serikali yake itachukua umiliki wa meli hizo na kuashiria kwamba zinaweza kutumika kuhifadhi mafuta.

Tangu Disemba 10, Marekani imezikamata meli mbili za mafuta inazozituhumu kukwepa vikwazo vya Washington kwa biashara ya mafuta ya Venezuela.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amezitaja hatua hizo za Marekani kuwa "vitendo vya kijambazi na uharamia wa kimataifa".

Miezi ya karibuni, utawala wa Trump umezidisha shinikizo kwa serikali ya Maduro inayomtuhumu kufadhili biashara haramu ya dawa za kulevya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW