1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Trump: Mipango ya waandamanaji kunyongwa Iran imesitishwa

15 Januari 2026

Idadi ya vifo kufuatia maandamano yanayoendelea kuitikisa Iran imeongezeka na kufikia watu 3,428, hayo ikiwa ni kulingana na shirika la haki za binadamu la Iran.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei
Kiongozi Mkuu wa Iran Ali KhameneiPicha: DW

Maandamano hayo yamezusha pia hali ya wasiwasi baada ya Marekani kutishia kuingilia kati na Iran ikionya kuwa italipiza kisasi. Marekani imeanza kuwaondoa wanajeshi wake katika kambi zilizopo Mashariki ya Kati, huku Uingereza ikitangaza kuufunga kwa muda Ubalozi wake mjini  Tehran.

Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump amesema jana usiku kuwa amepewa "taarifa zenye kuaminika" kwamba mipango ya serikali ya kuwanyonga waandamanaji waliokamatwa imesitishwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kwa sasa hali imedhibitiwa huku akiishutumu Israel kutaka kuiingiza Marekani vitani kwa niaba yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW