1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump na mkewe waambukizwa virusi vya corona

2 Oktoba 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa yeye na mkewe Melania Trump wameambukizwa virusi vya corona. Kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wa Twitter, Trump amesema kwa sasa yeye na mkewe wanakwenda karantini.

USA Washington Donald Trump und Melania
Picha: Andrew Caballerro-Reynolds/AFP/Getty Images

Trump mwenye umri wa miaka 74 yuko katika kundi la watu wanaoaminika kuwa wanaweza kuathirika vibaya na virusi hivyo, kwanza kutokana na umri wake na pili kwa kuwa anadaiwa kuwa na uzani kupita kiasi. Rais huyo amekuwa na afya njema katika kipindi chote ambapo amekuwa rais ila hafanyi mazoezi ya mara kwa mara au kula chakula chenye afya. Awali Trump alipuuza virusi hivyo na mara kadhaa amenukuliwa akisema kwamba virusi hivyo vitaangamia tu. Zaidi ya watu laki mbili wamefariki kutokana na virusi vya corona Marekani huku idadi kubwa ikiwa wazee na watu waliokuwa na magonjwa mengine kabla ya kuvipata virusi hivyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW