Trump na Putin kufanya mazungumzo kwa njia ya simu
13 Januari 2025Matangazo
Mike Waltz, mshauri wa usalama wa taifa atakayeshika wadhifa huo mara tu Trump atakapoingia madarakani amethibitisha kuwepo kwa mpango huo na kwamba unafanyiwa kazi:
“Bado hatujaweka mpamgo kazi kamili wa mazungumzo hayo. Tunaufanyia kazi ila mazungumzo kwa njia ya simukati ya Trump na Putin yanatarajiwa kufanyika katika siku kadhaa au hata wiki zijazo." Watz alisema.
Soma pia:Trump aitaka NATO kutumia 5% ya Pato la Taifa kwa ulinzi
Trump atakayeapishwa kama Rais wa Marekani Januari 20 anajipambanua kama msuluhishi katika vita kati ya Urusi na Ukraine.
Wakati huo huo Ukraine imesema leo kwamba imezidungua droni 78 kati ya 110 zilizorushwa na urusi usiku wa kuamkia leo Jumatatu.