Trump sasa ahimiza upigaji kura kwa njia ya posta
5 Agosti 2020Maombi ya Wademocrat kutaka kupiga kura kupitia posta yameongezeka jimboni Florida, jimbo ambalo Trump kwa kiasi fulani ni lazima ashinde kujihakikishia muhula wa pili.
Wademocrat kwa hivi sasa wamepata wakaazi milioni 1.9 wa jimbo la Florida ambao wanataka kupiga kura kwa posta mwezi Novemba, karibu watu 600,000 zaidi kuliko Warepublican milioni 1.3, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa jimbo la Florida.
Katika mwaka 2016 , pande zote mbili zilikuwa na watu kiasi ya milioni 1.3 waliojiandikisha kabla ya uchaguzi mkuu.
'Iwapo utaiita kura kwa njia ya posta ama kura bila mwenyewe kuwapo, mfumo wa uchaguzi katika jimbo la Florida ni salama, uliokwisha jaribiwa na wa kweli," Trump aliandika katika ukurasa wa Twitter.
'Mfumo wa kupiga kura wa Florida umefanyiwa utaratibu wa usafi, tumeshinda juhudi za Wademocrat kuubadilisha, kwa hiyo katika jimbo la Florida nawahimiza wote walioomba karatasi za kupigia kura, wapige kura kwa njia ya posta.
Afisa anayehusika na masuala ya vyombo vya habari wa Ikulu ya White House Kayleigh McEnany alikataa hoja kwamba rais huyo kutoka chama cha Republican kwamba amebadili msimamo wake.
Sababu maalumu
Alisema Trump anaunga mkono kura bila mwenyewe kuwapo kwa njia ya posta kwa sababu maalum, wakati akipinga majimbo kutuma karatasi za kupigia kura kwa wapiga kura wote bila kujali iwapo wameziomba.
Maafisa wengi wa uchaguzi wanasema kuna tofauti ndogo sana kati ya upigaji kuwa bila kuwapo mahali pa kupigia kura na kupiga kura kutumia njia ya posta.
Trump alifafanua wiki hii juu ya kwanini anaunga mkono upigaji kura kwa njia ya posta jimboni Florida, lakini si kwingineko.
'Wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka mingi, na wamefanya vizuri sana,' alisema katika mkutano na waandishi habari.
Hii ilichukua miaka mingi kufanikisha hilo," ameongeza. "Hii haichukui wiki ama miezi. Suala hili na Nevada, watapiga kura katika muda wa wiki chache. Na huwezi kufanya bivyo."
Nevada yaruhusu upigaji kura wa Posta
Maafisa wa Nevada yamejiunga na majimbo mengine kadhaa ambayo yanapanga kutuma karatasi za kupiga kura kwa wapiga kura. Majimbo mawili, Califonia na Vermont, yamechukua hatua mapema majira ya joto mwaka huu kutumia sera za upigaji kura kwa kutumia posta moja kwa moja.
Mswada ulipitishwa na wabunge siku ya Jumapili, gavana wa jimbo la Nevada Steve Sisolak , kutoka chama cha Democratic, alitia saini mswada huo kuwa sheria siku ya Jumatatu.
Katika ujumbe katika ukurasa wa Twitter Trump aliuita upitishaji wa sheria hiyo, kuwa ni 'mapinduzi ambayo si halali ya usiku" na kumshutumu Sisolak kwa kutumia janga la virusi vya corona kuhakikisha kura zitakwenda kwa Wademocrats.
Chanzo: Reuters.